Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma maombi

Maombi yote yawasilishwe kwenye nyaraka isiozidi jumla ya karatasi 5 zitakazoonesha vigezo vya kipengele utakachoingia. Taarifa ziwe na muhimu ziambatane na nyaraka zingine za kuthibitisha taarifa hizo.

Kabla ya kuwasilisha maombi, tafadhali hakikisha
 • Vitendo vyote vilivyojumuishwa vimetendeka ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.
 • Muombaji hana ulazima wa kuwa raia wa Tanzania, lakini shughuli husika lazima ziwe zimefanyika ndaji ya Tanzania
 • Tafadhali jitahidi kujibu maswali yote yatakayoulizwa na majaji na kuwepo na vithibitisho vyovyote vtakavyohitajika kuthibiisha majibu yako.
 • Tafadhali, ni muhimu kusoma vigezo na masharti.
 • Uwasilishwaji wa maombi
  Wakati wa kuwasilisha maombi, tafadhali hakikisha yafuatayo
 • Maombi yako yasizidi idadi ya karatasi tano(5) zenye ukubwa wa A4. Hakuna kitu kingine chochote kinachotakiwa Zaidi ya vielelezo vya kuthibitisha taarifa zilizo katika maombi yako mfano, picha, malengo na mikakati ya taasisi.
 • Fomu iliyopakuliwa kwa ajili ya kufanya maombi iambatanishwe na nyaraka za maombi
 • Maombi yawe yamechapwa kwa rangi
 • Umegusia kila kipengele cha maombi.
 • Maelezo mafupi kuhusu taasisi isiyozidi maneno 50, hii haiambatanishwi na nyaraka za maombi ila itahitajika kama sehemu ya maombi.
 • Picha mbili zinazoendana na kipengele chako cha maombi yenye ubora mkubwa ziwasilishwe kwenye CD au diski mweko
 • Nembo ya taasisi yako yenye kiwango cha juu. Hii iwasilishwe kwenye CD au diski mweko

 • Kumbuka: vipengele tajwa hapo juu vitahitajika katika uwasilishwaji wa maombi yako. Hakuna mabadiliko yoyote yatakayoruhusiwa baada ya kuwasilisha maombi yako. Ukubwa wa viambatanishi kwenye CD au diski mweko usizidi 8MB

  Peleka nakala yako kwenye ofisi za kimikoa za Chama cha Wenye biashara, Viwanda na Kilimo(TCCIA) zilizo karibu nawe au tuma kupitia;

   MAOMBI YA USHIRIKI TUZO ZA KILIMO 2019
   PKF East Africa.
   JENGO LA GIRL GUIDES, GHOROFA YA KWANZA
   MTAA WA KIBASILA, UPANGA
   S.L.P 7323, DAR ES SALAAM TANZANIA.