Kuhusu Tuzo Za Kilimo

KUSHEREHEKEA UFANYAJI KAZI MAHIRI, UBORA, UBUNIFU NA UWAJIBIKAJI KWENYE KILIMO

Tuzo za Kilimo inatambua na kusherehekea mashirika na wadau mbalimbali wanaoonesha ubunifu unaochangia nchi ya Tanzania kuonekana kiongozi kwenye sekta ya Kilimo kikanda. Vipengele mbalimbali kwenye tuzo hizi vinaakisi maeneo bora makuu kwenye sekta hii mahiri yakiwemo kilimo cha mazao, vinywaji, uzalishaji wa chakula na mengine mengi

Waandaaji

Biashara ya Kilimo ni moja ya sekta muhimu ya asili nchini Tanzania inayochangia takribani Dola za Kimarekani Bilioni 13.9 kwenye uchumi wa nchi huku ikitoa ajira kwa zaidi ya asilimia 67 ya wananchi moja kwa moja au kupitia njia nyinginezo.

Programu hii ya Tuzo pia ni jukwaa la kuonesha juhudi za wadau mbalimbali wanaochangia kwenye maendeleo na kusherehekea pamoja nao mafanikio yao kupitia tuzo hizi

Kampuni ya 361 Degrees ikiungana na chama cha wenye Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) pamoja na kampuni ya PKF East Africa kwa mara ya kwanza ndani ya nchi na kikanda imejipanga kusherehea mashujaa hawa wasiotambulika ambao wameshinda vikwazo mbalimbali katika kuwawezesha wananchi wa Tanzania na nje ya mikapa huku ikizalisha mapato kwa nchi.

Wakulima wa kitanzania wamekuwa ni moja ya watu wasio na bahati. Kutoka kwenye usambazaji na bei ya mbolea isiyoridhisha kwenye siku za karibuni hadi kwenye ucheleweshwaji wa utoaji wa pembejeo za kilimo kama vile mbegu ambayo umekuwa ukiathiri misimu ya upandaji na mavuno, na ukosekanaji wa masoko yaliyo tayari lakini pamoja na hayo yote, wakulima wamekuwa wakijidhatiti vyema katika kukabiliana na changamoto hizo huku wakiendeleza vyema biashara na sekta hiyo

Kampuni ya 361 Degrees ikihamasishwa na utendaji bora wa wadau wa sekta hii ya kilimo, imefikiria kutengeneza mfumo wa utoaji wa tuzo wa kila mwaka katika kusherehekea mashujaa hawa wasiotambulika. Hivyo tunatatakiwa kurudisha heshima ya ardhi yetu na kuthamini mchango mkubwa kwenye uzalisha wa chakula kwa mamilioni ya familia nchini Tanzania na nje ya mipaka

Itakuwa ni jukumu la pande zinazohusika na shindano kwenye kutoa taarifa za kiwango cha uwekezaji wao na mauzo yao ya mwaka. Ili kuonesha kuwa aina ya kilimo chao ni cha kipekee na chenje tija, washindani watapangwa kwenye madaraja tofauti kutokana na kujitolea kwao kwenye ulindaji wa mazingira, taratibu za kupunguza athari za mabadiliko ya tabia za nchi na maboresho ya maeneo ya ufanyaji kazi pamoja na vigezo vingine. Taasisi binafsi na za umma zinahimizwa kushiriki kwenye tuzo hizi

Kumekuwa na dhana kuwa ili kukishiriki kwenye tuzo kama hizi, mshiriki unatakiwa uwe bora na mwenye uwezo mkubwa kwenye sekta, ila Tuzo hizi za Kilimo zina dhamira tofauti ya kuonesha ubunifu na mabadiliko bila kujali ukubwa wa biashara ya washiriki

Tuzo hizi za Kilimo zimepangwa kufanyika jijini Dar es salaam mwezi wa Aprili 2019. Uchaguzi wa tuzo utafanywa na jopo mahiri la majaji likisimamiwa na kampuni mbia ya ukaguzi, PKF East Africa

 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Matunda na Mboga
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Mazao mchanganyiko ya Biashara
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Ushirika
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Vifaa na mashine
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Wafanyabishara
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Wanawake
 • Biashara bora ya Kilimo ya mwaka Wazalishaji wa Chakula na Vinywaji
 • Chipukizi kwenye Biashara ya Kilimo
 • Mafanikio bora ya mwaka
 • Mkulima bora mwanamke wa mwaka
 • Mkulima bora wa mwaka
 • Shamba kubwa ya Mwaka (Zaidi ya Mil 100)
 • Shamba ndogo ya Mwaka (Chini ya Mil 100)
 • Ubora kwenye Afya na Usalama
 • Ubora kwenye Elimu na Mafunzo
 • Ubora kwenye usafirishaji nje ya nchi
 • Ubunifu kwenye Biashara ya Kilimo
 • Uwajibikaji bora kwa jamii wa mwaka
 • Vijana bora kwenye Kilimo