Waamuzi na uamuzi

Jopo huru la waamuzi lililobobea katika maswala ya kilimo litatoa uamuzi juu ya washindi wa tuzo za kilimo.

Lengo letu ni kuwa na usawa katika uamuzi utakaokuwa na tathmini kutoka kwa wataalam wa sekta ya kilimo watakaotumia utashi na uzoefu wao wa kazi katika kufanya maamuzi hayo. Hii itahakikisha kwamba washindi wote ni kweli na ni haki wao kuwa washindi wa tuzo husika.

Jopo linachaguliwa kwa kulenga katika uamuzi wa huru na haki. Waamuzi wanaongozwa kwa kiapo cha usiri ambacho kitawaamuru kufanya kazi kwa haki na usawa. Kitendo hiki kipo chini ya usimamizi wa PKF East Africa, moja kati ya makampuni makubwa ya ukaguzi hapa Afrika Mashariki.

Tunatambua na kuheshimu taarifa muhimu za waombaji zilizowasilishwa wakati wa kufanya maombi. Taarifa hizo hazitatolewa nje ya jopo la waamuzi. Hatutachapisha jina la mtu au kampuni wala taasisi ambayo haikuchaguliwa kuwania tuzo yoyote, wala kutumia taarifa zozote bila idhini yako.
Shughuli pana ya uamuzi imeweka pamoja hatua za kufanya maamuzi

Shughuli ya uamuzi
  1. Baada ya maombi yote kuwa yamepokelewa, washiriki watatumiwa taarifa za tathmini za mwanzo.
  2. Maombi yote yatachunguzwa kwa umakini mkubwa na jopo la wakaguzi ili kubaini endapo wana vigezo vya kuwepo kwenye kipengele husika.
  3. Wahitimisho wa vipengele vyote watatangazwa kwenye tovuti ya tuzo.
  4. Waamuzi wamegawanywa katika makundi mawili ili kuepusha mgongano wowote unaoweza kujitokeza.
  5. Waamuzi watatoa viwango vya maombi yaliyopokelewa kwenye makundi ya viwango vilivyotangulizwa.
  6. Viwango vitajumuishwa, na mshiriki atakayepata kiwango cha juu atatangazwa mshindi wa kipengele husika.
  7. Washindi watatangazwa usiku wa ugawaji wa tuzo. Maamuzi wa waamuzi wetu ni ya mwisho na hayawezi kupingwa kokote kwa njia ya simu, barua pepe au njia yoyote ya mawasiliano.