TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Uzinduzi wa Tuzo za Kilimo kufanyika
  • Wadau wa kilimo kutunukiwa Tuzo
  • Shindano la Tuzo za Kilimo lafunguliwa.

TUZO za kwanza za kilimo nchini zitakazoshindanisha vipengele 40 katika sekta ya kilimo hasa kwa kuangalia ubunifu, ubora na kujitoa kwa wadau wa sekta hiyo ziitafanyika mnamo April mwaka huu.

Tuzo hizo zinalenga kuwajenga uwezo na kuwaweka karibu zaidi wadau hao wa kilimo ambayo ni sekta inayochangia uchumi wan chi ikiwa imetoa ajira kwa asilimia 67 ya wananchi huku ikichangia takribani Dola za Kimarekani Bilioni 13.9. Tuzo hizo zinalenga kuwatambua na kuwatunuku vinara katika kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyo ambao wameleta mchango chanya katika kuifanya Tanzania kuwa kinara katika sekta ya kilimo.

Akizungumzia Tuzo hizo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCCIA Fatuma Hamis alisema kuwa hiyo ni nia mojawapo ya kutanua wigo wa ubunifu na kuwavutia watu wengi zaidi kupenda kilimo kwa kuwa wanapewa motisha,wanawezeshwa na kuwaongezea ubunifu katika nyanja mbalimbali kwenye kilimo.

Alisema,“TCCIA imefurahi na kujisikia yeney furaha kwa kuwa sehemu ya Tuzo hizo kwenye sekta ya kilimo na mnyororo mzima wa thamani, hii ni kwa mara ya kwanza kutokea hapa nchini na hakika zitaendelea kuwavutia watu ambao tayari wamekuwa wakisaidia kuikuza sekta hii kuendelea kufanya hivyo huku pia kizazi kijacho kikivutiwa kujikita kwenye sekta hii na kuitumia katika kuiendeleza nchi kwa miaka ijayo”

Aliongeza, kuna mafaniko makubwa yanayoweza kupatikana kupitia kilimo biashara ambapo yatachangia kwa kiasi kikubwa kufikia Tanzania ya uchumi wa kati unaotegemea viwanda kama ambavyo Rais, Dk John Magufuli amekuwa akisisitiza.

Alisema“Kilimo kimekuwa na uwezo wa kutoa mazao yanayoendana na malighafi iliyotumiwa kuzalishia ambapo inaweza kutumiwa kama malighafi katika viwanda mbalimbali nchini.

Aliongeza kuwa ndio maana tuzo hizo zimeamua kutenga vipengele 20 ili mwisho wa siku kila anayefanya vema kwenye kitu fulani kwenye sekta hiyo atapata tuzi.

Aliongeza kuwa uchaguaji wa nani ashinde kwenye kipengele gani kwenye tuzo hizo utaendeshwa na jopo la wataalamu litakalosimamiwa na kampuni kubwa la Africa Mashariki PKF ambapo inajihusisha na masuala ya ukaguzi na ushauri wa biashara.

Mchakato rasmi wa utolewaji wa tuzo hizo utaanza Machi 25 na kuishia usiku wa Aprili 15 ambapo wakulima, kampuni za masuala ya kilimo, mashirika na mtu au watu walioko wanaweza kushiriki na kuwa fomu zinapatikana kwenye ofisi za TCCIA nchini na kwenye mtandao wa kijamii

Tuzo hizo zinaletwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture, 361 Degrees na PKF East Africa.

  • Phone: +255-676-303880