Sera ya usiri;

Tumeandaa sera hii ili kuonesha kujifunga kwetu na usiri juu ya taarifa utakazotupatia. Tunajidhatiti juu ya usiri wa taarifa utakazotupatia pamoja na kuhakikisha kwamba unapata kilicho bora kutoka kwenye tovuti yetu. Endapo utakuwa na maombi binafsi kuhusiana na taarifa zako binafsi au maulizo mengine yanayohusiana na sera hii ya usiri tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe info@361africa.com

Sera hii ya usiri itahusika kwenye taarifa zote binafsi utakazotupatia kama inavyoelezwa hapa Tanzania kwenye kanuni za ulinzi wa taarifa. Katika sera hii ya usiri tunaeleza taarifa binafsi kama taarifa au taarifa binafsi. Hatutahusika na usiri au utaratibu wowote wa taarifa kutoka katika tovuti yoyote ambayo utaweza kuitumia katika mwendelezo wa kutumia tovuti hii kwa njia ya kiungo cha tovuti au njia nyingine.

Taarifa zitakazo kusanywa na matumizi yake

Tunakusanya taarifa zako binafsi katika ngazi mbalimbali katika utumiaji wako wa tovuti hii pindi tu utakapojisajili kwetu. Tunakusanya taarifa hizi katika kuhakikisha kwamba huduma zetu zinatolewa kwa ufanisi mkubwa kadiri inavyowezekana na hivyo kuweza kutimiza makubaliano yetu na wewe.

Tunaweza kutumia taarifa zako katika kufanya yafuatayo

 • Kuingiza taarifa zako katika mfumo wetu wa kumbukumbu hivyo kurahisisha utendaji wetu.
 • Katika kufanya ukaguzi(mfano masoko, wateja na huduma) ili kutuwezesha kufanya kumbukumbu na kuendeleza huduma zetu pamoja na kukupatia wewe pamoja na wateja wetu taarifa za kweli kuhusu huduma zetu.
 • Kurahisisha mawasiliano baina yako na watumiaji wengine endapo itahitahika katika mtandao.
 • Tutakupa taarifa juu ya huduma na bidhaa ambazo kwa namna moja au nyingine tutaona ni za manufaa kwako kwa kutumia njia zifuatazo
 • Barua pepe
 • Simu
 • Ujumbe mfupi wa maneno na njia nyingine za ujumbe wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na ujumbe wa picha.
 • Sanduku la posta.
 • Barua pepe
 • Njia nyingine za mawasiliano mtandaoni.
 • Usalama

  Wakati tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha usalama wa taarifa unakuwepo, hatuwezi kuwahakikishia usalama dhidi ya matumizi mabaya ya vifaa vya tarakilishi na wachuuzi au matumizi mengine yasiyofaa. Unakubaliana na athari zozote zinazowea kujitokeza katika vitendo hivyo na hatutahusika kwa lolote endapo vitendo hivyo vitatokea.

  Maelezo

  Bila kuhusisha matumizi mengine yaliyo nje ya sera hii ya siri, hatutatoa maelezo yoyote juu ya taarifa tunazotunza kukuhusu kwa mtu yoyote isipokuwa tukitakiwa kufanya hivyo na polisi au mamlaka yoyote ya serikali kutoa taarifa zozote zinazokuhusu kuhusiana na matumizi yako ya tovuti hii. Mbali an hayo, tutatoa maelezo ya taarifa zako juu ya matumizi yako ya tovuti hii zikihitajika kwa mujibu wa sheria au zikihitajika na mtu mwingine juu ya vitendo vyovyote vitakavyoashiria uvunjwaji wa haki zao ambazo binafsi tutaona zina tija kutokana na matumizi yako ya tovuti hii.

  Vidakuzi vya tovuti

  Vidakuzi ni masharti ya taarifa ambayo tunaweza kutumia muda mwa muda katika kivinjari kwenye tarakilishi yako ili kutuwezesha kutunza kumbukumbu zako endapo unarudi kwenye tovuti. Kwa kuongezea, tunatumia vidakuzi ili kutusaidia katika upatikanaji wa watumiaji wasiojulikana, takwimu zilizounganishwa pamoja na uchambuzi wa wageni wetu kwa kutumia huduma za kiuchambuzi za Google. Tunaweza pia kutumia vidakuzi katika kuhakikisha unafurahia huduma za tovuti yetu na kuboresha huduma zetu kwako. Endapo ungependa, waweza weka mipangilio ya kivinjari chako isiruhusu vidakuzi. Ikumbukwe kwamba waweza ukajitoa katika huduma za kiuchambuzi za Google na matangazo kwa kuweka mipangilio ya kivinjari chako vile upendavyo. Ukifanya hivyo waweza bado kutumia tovuti yetu lakini haitakupa urahisi wa kufanya baadhi ya mambo. Mipangilio ya kivinjari inategemeana na mfumo wa mtandao ulio katika kifaa chako.

  Vidakuzi havina taarifa kama anuani yako, namba zako za simu au taarifa za kadi za kufanyia malipo na hatutatoa taarifa za vidakuzi kwa watu wengine.

  Upatikanaji wa taarifa;

  Endapo katika hatua yoyote ungepena kutengeneza au kuhakikisha taarifa zako tulizonazo, tafadhali wasiliana na sisi kwa kutuma barua kwenye anuani yetu ya biashara. Tunayo haki ya kuchukua hatua stahiki kuhakikisha utambulisho wako kabla ya kutoa taarifa zozote tulizonazo.

  Mabadiliko ya sera ya usiri

  Mabadiliko yanaweza kufanyika katika sera hii ya usiri kutokana na muda na mabadiliko yaliyofanywa yatatangazwa kwenye tovuti yetu mara moja.